
“Nilienda shule mara ya kwanza Lushoto mwaka 1956, nilikuwa napenda kucheza sana, mwalimu akasema kesho usije shule nikaona sawasawa tu. Rafiki yangu yeye alikuwa hajaanza nikaacha shule mpaka niliporudi tena” – Rais Mstaafu Jakaya Kikwete
“Ni kweli kwamba watu wetu hawasomi sana, hata magazeti wanasoma vichwa vya habari tu. Mimi nilijua kusoma na kuandika baada ya kwenda shule” – Rais Mstaafu Jakaya Kikwete
“Nilipomaliza Sekondari nikaenda Kibaha Form 5 na 6 baada ya hapo nikaenda Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1975” – Rais Mstaafu Jakaya Kikwete
“Mke wangu wa kwanza mama yao wakina Ridhiwan, Mungu amrehemu. Ilikuwa siku moja tumetoka na baba tukaingia nyumba 1 tukamkuta msichana tukabaki tunatazamana tu. Tulivyorudi baba akasema umemuonaje yule msichana” – Rais Mstaafu Jakaya Kikwete
You must be logged in to post a comment.