BABA AMCHARAZA FIMBO MWANAE MPAKA KUFA

Polisi Kagera wamethibitisha kutokea kwa kifo cha Mtoto wa Darasa la 4 kilichosababisha na kupigwa na Baba yake, chanzo ni kwenda matembezi ya sikukuu juzi bila ruhusa ya Wazazi.

Jeshi la polisi mkoani Kagera, linamshikilia Amos Rudovick (39) kwa tuhuma za kusababisha kifo cha mtoto wake Dastan Amos (13), kwa kumchapa na fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake na baada ya uchunguzi ilibainika kuwa alimvunja shingo na uti wa mgongo.

Kamanda wa Polisi Kagera Revocatus Maliki amesema “Alimchapa bila huruma maeneo mbalimbali na kwa kutumia fimbo yenye unene mkubwa”

“Uchunguzi wa kitabibu umefanyika na kubaini kwamba Marehemu alivunjika shingo na uti wa mgongo na ndicho kilichothibitishwa na Wataalamu wa Afya kwamba ndio chanzo cha kifo cha huyu Mwanafunzi, Jeshi la Polisi linafanya kazi yake”

Mwanamke aitwae Jesca Samson (37) wa Kagera amejiua kwa kunywa sumu ya panya baada ya ugomvi wa muda mrefu kidogo na Mumewe, siku ya kujiua Jesca alimnywesha sumu Mtoto wao pia lakini amenusurika kifo.

Polisi Kagera wamesema “Kabla ya kifo, Jesca na Mume wake aitwae Samson walikua na mzozo, mgogoro wa kifamilia ambapo Samson aliuza kipande cha ardhi bila kumshirikisha Mke wake, baada ya Mwanamke kufahamu alimlalamikia”

“Ni kesi ambayo ilisababisha ugomvi mwingine mpaka Mwanaume kupelekwa Mahakamani Mahakama ya mwanzo na kukaa gerezani kwa muda wa miezi kama mitatu”-Polisi, Kagera.