TRA YA KUSANYA TROLIONI 2.088

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Dr. Edwin Mhede leo January 1 2021 amesema mamlaka hiyo kwa December 2020 imepata mafanikio ya kukusanya Trilioni 2.088.

“Tulikua na lengo la kukusanya fedha taslimu Trilioni 2.072 kwa December 2020 lakini tumekusanya Trilioni 2.088 ikiwa ni sawa na ufanisi wa asilimia 101 ya lengo hilo, makusanyo haya ni ya kihistoria, hatujawahi kukusanya fedha kiasi hicho toka TRA imeanzishwa”

“Tunamshukuru Mungu lakini kwa kiasi kikubwa tunawashukuru Walipa kodi, tunawapongeza kwa kutimiza wajibu wenu mtukufu na wa kisheria ambao kwakweli kupitia uletaji kodi hizo za hiari tumefikia hapo” – Dr. Edwin Mhede, Kamishna Mkuu TRA, video nzima itazame hapa