Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 26.12.2020

Erling Braut Haaland

Mkufunzi wa zamani wa Tottenham Hotspur Mauricio Pochettino anataka kumleta mshambuliaji wa Barcelona na Argentina Lionel Messi, 33, Paris St-Germain. Pochettino anapigiwa upatu kuchukuwa wadhifa wa ukufunzi katika klabu hiyo ya bingwa ya Ufaransa baada ya Thomas Tuchel kufutwa Alhamisi. (Le Parisien – in French)

Kiungo wa kati wa England Dele Alli, 24, huenda akaondoka Spurs wakati Pochettino atakapojiunga na klabu ya Ligue 1. (Sun)

Jurgen Klopp amwambia Mohamed Salah sababu pekee ya kuondoka Ligi ya Primia ni hali ya hewa

Chelsea wanajiandaa kuungana na Real Madrid, Bayern Munich, Manchester United na Manchester City katika kinyang’anyiro cha kumsaka mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway Erling Braut Haaland, 20. (Sky Italia, via Mail)

Juventus na AC Milan wameingi akatika kinyang’anyiro cha kumsaka mshabuliaji wa Celtic Mfaransa Odsonne Edouard, 22. (Calciomercato, via Sun)

Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp amemwambia mshambuliaji wa Misri Mohamed Salah sababu pekee ya kuondoka Ligi ya Primia ni hali ya hewa lakini amekubali kuwa klabu hiyo haiwezi kumlazimisha mchezaji kusalia nao bila hiari yake. (Guardian)

Kiongo wa kati wa Arsenal Mjerumani Mesut Ozil, 32, amefany amazungumzo ya siri na Fenerbahce katika juhudi za kutaka kuondoka Gunners. (Bild – in German)

Ozil ana uhakika hataregeshwa katika kikosi cha kwanza cha Arsenal nusu ya pili ya msimu na hakuna uwezekano wa kuhamia Marekani. (INews