
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Mohamed Dewji ‘Mo’, ameahidi kutumia zaidi ya Sh milioni 500 ili amshushe straika mpachika mabao atakayeingia moja kwa moja kikosi cha kwanza ambapo ametajwa kuwa ni staa wa Orlando Pirates, Jean Makusu, na imeelezwa kuwa wapo kwenye hatua nzuri.
Pamoja na Makusu kuwa kwenye mkataba na timu ya RS Berkane ya nchini Morocco akiwa anaichezea Orlando kwa mkopo, bado Mo amevutiwa naye japo dau lake likitajwa kufi kia Sh milioni 800, ambazo Mo amekubali kutoa nusu au robo tatu ya kiasi hicho cha fedha.
Mkataba wa Makusu unatarajiwa kufi kia ukingoni Juni, mwakani, hii ni kwa taarifa ya umiliki wake ambayo ni Kampuni ya Bro Management ambayo ina wamiliki pia wachezaji wengine wa Ligi Kuu Bara, Mukoko Tonombe wa Yanga na Clatous Chama wa Simba.
Watch “KIKUNDI CHA SANAA ASILI YA MARA KUTOKA BUTIAMA” on YouTube https://youtu.be/euiqiTKuU1w
You must be logged in to post a comment.