
Rais Dkt John Magufuli leo ameungana na Waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Imakulata Chamwino mkoani Dodoma kusali Misa Takatifu ya Krismasi ambayo ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo.
Baada ya Misa hiyo iliyoongozwa na Paroko wa Parokia hiyo Padre Paul Mapalala, Rais Magufuli amewapongeza na kuwatakia heri Watanzania wote kwa sikukuu ya Krismasi na amewataka kuendelea kumshukuru Mungu kwa miujiza na upendo mkubwa anaolitendea Taifa la Tanzania.
Amesema upendo na miujiza ya Mungu kwa Tanzania inajidhihirisha katika kipindi hiki ambapo dunia inapita katika wakati mgumu wa janga la ugonjwa wa Corona ambapo maelfu ya watu wanaendelea kupoteza maisha kila siku, lakini Tanzania imeepushwa na janga hilo na maisha ya Watanzania yanaendelea kama kawaida
You must be logged in to post a comment.