
Lloyd Austin, Jenerali mstaafu wa jeshi la ardhi la Marekani amekuwa mtu mweusi wa kwanza kuteuliwa kuwa waziri wa Ulinzi wa Marekani.
Hata hivyo, Lloyd aliyestaafu utumishi wa jeshi mwaka 2016, bado hajatimiza miaka 7 ya kisheria tangu kustaafu uongozi wa jeshi hadi kustahili kuwa kingozi wa kiraia. Kwa sababu hiyo, uteuzi wake utatakiwa kuthibitishwa na bunge (Congress) ambalo lina uwezo wa kuiweka pembeni sheria hiyo ya mwaka 1947 kwa maslahi ya Marekani.
Jenerali Lloyd Austin anatajwa kama mtu mkimya asiyependelea kuzungumza masuala ya kijeshi hadharani.
Amekuwa Kamanda wa majeshi ya Marekani nchini Iraq ambako alikuwa Kamanda mkuu wa pili kutoka juu.
Lloyd ndiye aliyeongoza mchakato wa kuondoa majeshi ya Marekani nchini Iraq wakati wa utawala wa Barack Obama, kisha akateuliwa kuwa mkuu wa kamandi malum (CENTRAL COMMAND) ya kijeshi inayosimamia maslahi ya kiusalama ya Marekani katika nchi zilizopo Pembe ya Afrika, nchi za kiarabu na Asia ya kati.
Uteuzi wa Jenerali Lloyd katika nafasi ya Uwaziri wa Ulinzi wa Marekani unatoa ishara gani katika utawala wa Rais Joe Biden?
Kama ilivyokuwa kwa uteuzi wa waziri wa Mambo ya kigeni Bw. Antony Blinken, uteuzi huu unalenga kudumisha mahusiano ya Marekani na marafiki zake, na zaidi kuongeza ushawishi wa Marekani duniani – ili kujenga pale alipoharibu Donald Trump.
“America is stronger when it works with its allies”. Ni kauli ya Rais Mteule Joe Biden, ambayo imerudiwa na Jenerali Lloyd Austin alipotoa hotuba fupi baada ya uteuzi wake.
“Marekani inakuwa na nguvu zaidi inapofanya kazi pamoja na washirika wake”. Ndio imani ya Joe Biden na wateule wake.
Uteuzi wa Lloyd Austin umeungwa mkono na waziri wa Ulinzi wa zamani Robert Gates na waziri wa masuala ya kigeni wa zamani Collin Powell.
You must be logged in to post a comment.