KICHUYA AFUNGIWA MIEZI 6, SIMBA KULIPA ZAID 290

Shirikisho la soka duniani Limemfungia Miezi 6 Aliyekuwa Mchezaji Wa Zamani Wa Simba Na Pharco Ya Misri kwa Kosa La Kuihama Klabu Yake Ya Pharco Bila Kufuata Taratibu Za Uhamisho. Kichuya Tayari Ameshachezea Klabu Mbili Za Tanzania Bila Ya Kuwa Na Kibali Cha Uhamisho (Release Later) Ambazo Ni Simba Na Sasa Namungo Ya Mkoani Lindi.
Taarifa zinasema FIFA imemfungia winga wa zamani wa simba, Shiza Kichuya miezi sita kucheza soka kutokana na suala lake la kuihama klabu yake ya Pharco ya Misri mapema mwaka huu.
Sababu ni kutokana na klabu yake ya Pharco kushitaki FIFA baada ya SHIZA kuondoka bila kufuata taratibu za uhamisho,Shiza ameshazitumikia klabu mbili za nchini Tanzania bila kufuata uhalali (vibali vya kazi-Release letter) ambazo ni Simba sc na Namungo.
Inaelezwa Klabu ya Simba imepigwa Faini Ya Dola Za Kimarekani $130,000 Sawa Na Zaidi Ya Shillingi Milioni 290 Za Kitanzania.
You must be logged in to post a comment.