MAYWEATHER 2021 KUPANDA ULINGONI TENA

Floyd Mayweather ambaye alistaafu ndondi kisha kurejea tena ulingoni mwaka 2017 kwa kupigana na Conor McGregor, kisha mwaka 2018 akapigana na Tenshin Nasukawa, sasa ametangaza rasmi Februari 2021, atapigana pambano la maonyesho maalum dhidi ya Logan Paul.

Logan Paul ni mkali wa maonyesho kwenye mtandao wa YouTube na amepigana pambano moja la ulingoni ambapo alipigwa na KSI Novemba 2019.