
Mtoto Braulio Ramirez (17) wa Mexico anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuwaua Wadogo zake wawili wa kike, Diana (7) na Guilleri (12) ili kulipa kisasi kwakuwa Mama yake anawapenda sana Wadogo zake kuliko yeye.
Braulio anaishi na Baba yake, siku ya tukio alitembelea nyumbani kwa Mama yake Erica (38) na alipoachwa akae na Wadogo zake kwa saa chache Mama alipotoka akatekeleza mauaji hayo.
Mama aliporudi akakuta Watoto wanavuja damu safakuni na alipotaka kupiga kelele na yeye pia akasukumwa kisha Mtoto akaondoka akiwa na Bastola Mkononi, Braulio atahukumiwa kama Mtu mzima mwakani kwakuwa atakuwa na miaka 18.
You must be logged in to post a comment.