ACT-WAZALENDO| KUSHIRIKI SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA

“Kamati Kuu kwa kuzingatia Ibara ya 9(3) ya Katiba ya Zanzibar imeridhia ACT kushiriki kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar na imeielekeza Kamati ya Uongozi kupendekeza jina la Mwanachama atakayekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar” -Ado Shaibu, Katibu Mkuu ACT

“Kamati kuu ya ACT Wazalendo imeazimia wawakilishi wachache (Madiwani, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Wabunge) ambao wametangazwa kushinda Uchaguzi Mkuu, waruhusiwe kushiriki kwenye vyombo vya uwakilishi ili waendeleze mapambano”-Ado Shaibu