Uteuzi wa Baraza la Mawaziri Tanzania

Rais wa Tanzania,  John Magufuli leo Jumamosi Desemba 5, 2020 amefanya uteuzi wa mawaziri 21 na naibu mawaziri 23 huku akiwateua waliokuwa makatibu wakuu wa wizara kuwa wabunge na kisha kuwateua kuwa mawaziri.

Hii leo Baraza limetangwaza ambapo jumla ya Mawaziri 21, na kufanya idadi yao kuwa 23.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi, Mhandisi John William Kijazi amesema pia Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Naibu Mawaziri 23 na Makatibu Wakuu wa wizara mbalimbali.

Pia amewateua wabunge wawili ambao pia amewapa nafasi ya uwaziri.

Mawaziri Waliosalia Katika Nafasi 1:Profesa Joyce Ndalichako (Wizara ya Elimu) 2:Dotto Biteko (Wizara ya Madini) 3:Jenista Mhagama (Ofisi ya Waziri Mkuu) 4: Selemani Jaffo (Tamisemi) 5: George Simbachawene (Wizara ya Mambo ya Ndani) 6: Mwigulu Nchemba (Wizara ya Katiba na Sheria) 7: William Lukuvi (Wizara ya Ardhi) 8: George Mkuchika (Utumishi), 9: Medard Kalimani (Wizara ya Nishati).

BARAZA LA MAWAZIRI JIPYA LINA JUMLA YA WIZARA 23

  1. Wizara ya Ardhi-William Lukuvi
  2. Wizara ya Ulinzi na JKT Elias John Kuandikwa
  3. Wizara ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Capt Mstaafu George Mkuchika
  4. Wizara ya Maji -Juma Aweso
  5. Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo- Innocent Bashungwa
  6. Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana na wenye ulemavu – Jenister Mhagama
  7. Wazira ya Afya, maendeleo ya jamii,jinsia na watoto Doroth Gwajima (Mbunge mpya alikuwa naibu katibu mkuu)
  8. Wizara anayesimamia Uwekezaji ofisi ya Rais Mkumbo Kitilya
  9. Wizara ya Katiba na sheria Mwigulu Nchemba
  10. Wizara ya Ofisi ya Rais TAMISEMI Suleiman Jaffo
  11. Wizara ya Madini Dotto Biteko
  12. Wizara ya Nishati Dkt Medard Kalemani
  13. Wizara Ujenzi na Uchukuzi mbunge mpya Mhandisi Dkt Leonard Chamuliho (alikuwa Katibu Mkuu Uchukuzi)
  14. Wizara ya Kilimo Prof.Adolph Mkenda.
  15. Wizara ya Viwanda na Biashara Mwambie Geofrey Idelphonce.
  16. Wizara ya Mambo ya ndani George Simbachawene.
  17. Wizara ya Muungano na Mazingara Ummy Mwalimu.
  18. Wizara mpya ya Mawasiliano na Teknolojia na habari Dkt Faustine Ndugulile.
  19. Wizara ya Fedha Dkt Philip Mpango
  20. Wizara Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof Paramagamba Kabudi
  21. Wizara ya Maliasili na Utalii DK Ndumbalo Damas
  22. Wizara ya Mifugo na Uvuvi – Mashimba Mashauri Ndaki
  23. Wizara ya Elimu na Sayansi Prof Joyce Ndalichako