Joe Biden| Siku 100 za kuvaa Barakoa

Rais mteule wa Merika Joe Biden amesema kuwa atawaomba Wamarekani wavae Barakoa kwa siku zake 100 za kwanza ofisini ili kupunguza kuenea kwa virusi vya corona.

Biden amesema kuwa anaamini kutakuwa na upunguaji mkubwa wa kesi za Covid-19 ikiwa kila Mmarekani atavaa Barakoa.

Bwana Biden pia amesema ataamuru Barakoa zivaliwe katika majengo yote ya serikali ya Marekani.

Marekani imeripoti kesi milioni 14.1 na vifo 276,000 kutokana na Covid-19 hadi sasa.

Katika mahojiano na Jake Tapper wa CNN, Bwana Biden amesema: “Siku ya kwanza nikiwa madarakani nitakwenda kuuomba umma kwa siku 100 kuvaa Barakoa . Siku 100 tu za kuvaa Barakoa, sio milele. Siku mia moja”

Biden anatarajiwa kuapishwa Januari 20, 2021 kuwa rais wa 46 wa Marekani.