
CHADEMA imepoteza heshima yake kwenye jumuiya ya kimataifa baada ya kukandamiza haki za kisiasa za wanawake wa chama hicho kwa kuwazuia viti maalum vya ubunge wanavyopewa kikatiba na sheria .
Katika harakati za kuilinda CHADEMA na kuimarisha upinzani nchini, Ujerumani inashirikiana na mfumo dume wa CHADEMA kula njama za kuichafua Serikali ya Tanzania.
Ujerumani imemuhakikishia kuwa wanawake wawili watakaoweza kufanikisha mpango huo wa siri kwamba atapewa ukimbizi wa kisiasa na kwamba kila mwezi atalipwa Dola za Kimarekani 10,000, atapewa nyumba ya kifahari ya kuishi na familia yake, bima ya afya na usafiri.

Wanawake hao wanapaswa kuwa miongoni mwa wabunge 19 walioapishwa kuchukua viti maalum vya CHADEMA kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wanawake hao watawajibika kutangaza hadharani kwamba Halima Mdee alipokea Shilingi Bilioni 1.9 kutoka CCM ili awashawishi wanawake 18 wa BAWACHA wakubali kuwa wabunge wa viti maalum kwa kumpa kila mmoja shilingi milioni 100 akiwemo nayeye katika mgao huo.
Taarifa za muda huu zinasema kwamba Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amempa kazi Askofu Shoo ili amtafute mmoja wa muumini wake mtiifu kutoka kwenye kundi la wabunge 19 kwa ajili ya kutekeleza uovu huo
Shoo anafanya kazi hiyo kwa kushirikiana na Upendo Peneza, ili kukamilisha misheni hiyo.
Peneza ameahidiwa kupewa Uenyekiti wa BAWACHA huku washirika wake wakiahidiwa kupokea mamilioni kutoka kwenye Ubalozi wa Ujerumani.
Kwa mujibu wa uchambuzi wetu, Ujerumani inaingilia siasa za Tanzania kwa lengo la kuvuruga umoja wa Watanzania kwa kuasisi misimamo mikali ya kisiasa pamoja na kuchanganya siasa na dini.


Tunautaka ubalozi wa Ujerumani uache mara moja mpango huo ambao unaweza kuhatarisha amani ya Taifa hilo la Afrika ambalo limepata maendeleo makubwa ndani ya miaka mitano iliyopita chini ya Rais Mhe. Dkt. John Pombe MAGUFULI.
You must be logged in to post a comment.