RAIS MTEULE WA MAREKANI KUIMARISHA USHIRIKIANO NA UN

Rais mteule wa Marekani Joe Biden amesisitizia kuimarishwa ushirikiano kati ya nchi hiyo na Umoja wa Mataifa katika masuala muhimu ya dunia.

Bwana Biden ametoa msimamo huo katika mazungumzo aliyofanya kwa njia ya simu na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana António Guterres.