UN | HABARI NJEMA KWA WAKULIMA NA WATUMIAJI WA BANGI

Tume ya Umoja wa Mataifa ya kudhibiti dawa za kulevya imeidhinisha pendekezo la Shirika la Afya Duniani (WHO) la kuondoa Bangi na utomvu wake kutoka kwenye kundi la dawa hatari zaidi zinazopaswa kudhibitiwa.

Hatua hii inafanya sasa Bangi itambulike kama mmea wenye mafunaa kwa ajili ya matibabu na itasaidia kukuza viwanda vinavyotengeneza dawa kwa kutumia bangi.

Taarifa ya UN imesema hii ni habari nzuri kwa Mamilioni ya Watu wanaotumia bangi kama dawa na pia ni hatua itakayosaidia ukuaji wa soko la bidhaa hiyo kwa misingi ya kimatibabu.