Dk. Mwinyi amesema hayo Ikulu Jijini Zanzibar, katika hafla ya makabidhiano ya fedha zilizotolewa na Wafanyabiashara watano wa Zanzibar kwa ajili ya ushiriki wa Timu ya Mlandege, kuelekea mchezo wa marudiano dhidi ya Timu ya CS Sfaxien ya Tunisia.
Alisema maendeleo ya michezo hapa nchini yatafikiwa kwa kuwepo udhamini wa uhakika utakaozinufaisha pande zote mbili kati ya wafanyabaishara na vilabu.
Aliwataka wafanyabiashara kote nchini kujitokeza kusaidia maendeleeo ya michezo, ikiwemo soka ili kurejesha hadhi ya mchezo huo iliyopotea.

Alisema kwa njia yoyote ile Taifa lina dhima ya kuhakikisha michezo inaimarika na kubainisha kuwa kamwe jambo hilo haliwezi kufikiwa bila ya kuwepo ufadhili ambapo Makampuni kwa utaratibu maalum yataweka fedha katika bajeti zao.
Dk. Mwinyi alisitiza umuhimu wa Wizara hiyo kusimamia mashindnao mbali mbali, akisema jambo hilo lina faida kubwa katika maendeleo ya michezo, kwa kigezo kuwa huongeza hamasa, kuinua kipato pamoja na kukuza utalii nchini.
Aidha, aliitaka Wizara hiyo kuendelea na juhudi za kutengeneza viwanja kila mahali, ili kuondokana na utaratibu wa timu kupokezana viwanja.
You must be logged in to post a comment.