RAIS WA ZANZIBAR AFANYA UTEUZI LEO

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt Hussein Ally Mwinyi

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt Hussein Ally Mwinyi amefanya uteuzi Wakuu wa Mikoa kama ifuatavyo :

  1. Idrissa Kitwana Mustafa, ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi.
  2. Ayoub Mohammed Mahmoud, ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja.
  3. Rashid Hadid Rashid, ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja.
  4. Salama Mbarouk Khatib, ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba.
  5. Mattar Zahor Masoud, ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba.