Video ya Nyimbo ya ‘WAAH!’Diamond Platnumz na Koffi olomide imeweka Rekodi Mpya Afrika

Video ya Nyimbo ya ‘WAAH!’ ya Staa wa muziki wa BongoFleva Diamond Platnumz aliyomshirikisha Legend wa Muziki Barani Africa koffi olomide imeweka Rekodi Mpya Afrika Baada ya Kufikisha watazamaji Million 1 kwenye Mtandao wa YouTube ndani ya Masaa 8.

Video hii ambayo imeachiwa rasmi Leo Novemba 30, 2020 inamfanya Diamond Platnumz kuwa Msanii wa kwanza (Sub Saharan) Kufikisha Views Milioni 1 Ndani Ya Masaa 8 katika mtandao wa YouTube

Diamond amevunja Rekodi ambayo awali ilikua inashikirikwa na Davido ambae alifikisha Views Milion 1 ndani ya Masaa 9 kupitia Video yake ya .

Rekodi hii inaendelea kudhihirisha ubabe na nguvu kubwa aliyonayo Diamond katika Muziki, kwasababu si rahisi wala mzaha kufikia namba za kutisha namna hii!