Wabunge wa viti maalumu chadema ni wabunge halali

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amewaapisha wabunge wateule Bw. Humphrey Polepole na Bi. Riziki Said Lulida kuwa wabunge kamili

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai amewaapisha Wabunge wawili wa Kuteuliwa na Mheshimiwa Rais, Mhe. Riziki Lulida na Mhe. Humphrey Polepole katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.

Akizungumza baada ya kuwaapisha wabunge wateule, Spika Ndugai amekemea vikali watu wanaodharau shughuli zinazofanywa na Bunge la Tanzania

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

“Waliokuwa na wasiwasi kuhusu wale Wabunge 19 (Halima Mdee na wenzake) sijui kuna hili kuna hili, niwatoe wasiwasi wale ni Wabunge kamili, na Wanahabari mkiwaandikia muwaite Waheshimiwa”-Spika wa Bunge, Job Ndugai

“Watanzania tupige vita na tukatae ukandamazaji dhidi ya Wanawake kwenye Jamii yetu kwa kisingizio chochote, Mbowe ni Rafiki yangu amesimama akaanza kuwatukana hadharani Wabunge hawa Wanawake ni aibu kuwatukana Wanawake hadharani”-Spika wa Bunge, Job Ndugai

Mh. Halima Mdee

“Mbowe umesahau Mdeee alivunjika mkono kwa ajili ya kukufuata Magereza, Bulaya apigwa akazimia amepelekwa Aga Khan kwa ajili yako Mbowe, Matiko amelazwa Segerea mara nyingi kwa ajili yako, mshahara wao kuwafukuza hadharani bila kuwasikiliza, haiwezekani”-Spika wa Bunge, Job Ndugai

“Kuna Mwanamke mmoja aligombea Morogoro amesimama na kuwaita wenzake covid 19 na yeye ni Mwanamke pia, hamjui wale 19 wamepitia matatizo gani, hamjui kwanini imekuwa hivyo, yapo mambo hatuwezi kusema, vipo vyama ni kampuni ya Mtu, Mtu ni Mungu Mtu”- Spika wa Bunge, Job Ndugai

“Nimuonye Mbowe na nimkanye mwenzangu asione sifa kwenye jambo hili, Wanawake ni Mama zetu, shangazi zetu, wanapokosea tuwatafute tukae nao sio kuwafukuza na kuona sifa, wale 19 ni wabunge labda itokee wajiuzulu au vipi ila sio kisa Mbowe na Mnyika wake, wale ni Wabunge”-Spika wa Bunge, Job Ndugai

“Mbowe analalamika Mwanachama wake Nusrat alikuwa Mahabusu, kwanini amechiwa na kuapishwa kuwa Mbunge, alitaka afie Magereza?, haya katoka sasa, uwe na Ndugu yako yupo kule imradi katoka si unamshukuru Mungu, yeye analalamika”- Spika wa Bunge, Job Ndugai

Bw. Humphrey polepole alikuwa Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM).
Bi. Riziki Said Lulida Akiapa mbele ya Spika