
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi leo amemuapisha Rashid Said Rashid kuwa Naibu Katibu Mkuu anaeshughulikia mifumo ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) katika Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango.
Hafla ya kuapishwa kiongozi huyo ilifanyika Ikulu Jijini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.


Katika maelezo yake mara baada ya kula kiapo Naibu katibu Mkuu alisema wananchi wanamatumaini makubwa na mabadiliko kwani wanahitaji kupata huduma nzuri na zilizo bora zaidi.
Alisisitiza kwamba teknolojia ya TEHAMA haitokuwa kwenye kodi pekee yake na badala yake itakwenda kwenye kila sekta ikiwemo uchumi wa buluu, huduma za afya, elimu na nyenginezo.

Alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha wananchi wanalipa kwa urahisi zaidi na kuepuka kwenda kulipa benki na kukaa muda mrefu ni lazima iondolewe ikiwa ni pamoja na kupata wepesi katika kufuatia masuala ya vyeti vya kuzaliwa.
Kabla ya uteuzi huo Naibu Katibu Mkuu huyo alikuwa Mkurugenzi wa Mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika benki kuu ya Tanzania.
You must be logged in to post a comment.