
Wabunge wa viti maalum kupitia chama cha upinzani cha CHADEMA wanaapishwa leo jijini Dodoma.
Wabunge hao 19 wameongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha)Halima Mdee kula kiapo cha uaminifu mbele ya Spika Job Ndugai.

Awali, Chadema iligoma kuteua wabunge wa viti maalumu wakidai kuwa hawatambui matokeo ya uchaguzi uliopita wakisema ulikuwa na kasoro lukuki. Uongozi wa chama hicho ulidai kuwa na kutuma wabunge wa vti maalumu ni kuhalalisha uchaguzi huo.

Katika uchaguzi wa mwezi uliopita, Chadema ilipata mbunge mmoja tu wa kuchaguliwa jimboni, Bi Aida Kenani kutoka jimbo la Nkasi Kaskazini mkoani Katavi.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai amewaapisha Wabunge 19 wa Viti Maalum kutoka CHADEMA katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.
Walioapishwa ni;
- Mhe. Halima Mdee
- Mhe. Grace Tendega
- Mhe. Ester Matiko
- Mhe. Cecilia Pareso
- Mhe. Ester Bulaya
- Mhe. Agnesta Kaiza
- Mhe. Nusrat Hanje
- Mhe. Jesca Kishoa
- Mhe. Hawa Mwaifunga
- Mhe. Tunza Malapo
- Mhe. Felister Njau
- Mhe. Naghenjwa Kaboyoka
- Mhe. Sophia Mwakagenda
- Mhe. Kunti Majala
- Mhe. Stela Fiayo
- Mhe. Anatropia Theonest
- Mhe. Salome Makamba
- Mhe. Conchesta Rwamlaza
- Mhe.Asia Mohammed.








You must be logged in to post a comment.