Zaidi ya Watu 30 wamepoteza maisha nchini Uganda na zaidi ya watu 500 wamekamatwa.

Msemaji wa serikali ya Uganda , Ofwono Opondo, amesema polisi wamechukua hatua stahili . Amewanyooshea kidole waandamanaji kwa kutotafuta “njia za amani” za kueleza na “kutatua” changamoto kwa kutumia njia za kisheria.

Wagombea kadhaa wa urais wamesitisha kampeni zao, wakitaka Bobi Wine aachiwe huru

Bobi Wine, jina lake halisi Robert Kyagulanyi, alikamatwa siku ya Jumatano kwa kukiuka masharti ya Covid, polisi walisema.

Anashutumiwa kukusanya makundi makubwa ya watu wakati wa kampeni Mashariki mwa nchi hiyo

Bobi Wine alikamatwa katika mkutano wa kampeni Jumatano akishtumiwa kwa kukiuka miongozo ya kudhibiti ugonjwa wa virusi vya corona kwenye mkusanyiko wa hadhara.

Hata hivyo Bobi Wine amepewa dhamana.

Mwanamuziki huyo ni miongoni mwa wagombea 11 wanaopambana na Rais Yoweri Museveni , ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 1986.

Rais wa sasa Yoweri Museveni ameendelea kufanya kampeni bila kukatizwa – wakati hajahutubia umati, wafuasi wake wamekuwa wakikusanyika kumkaribisha katika miji mbalimbali.

Rais wa Uganda na Mgombea Urais

Uchaguzi utafanyika tarehe 14 mwezi Januari mwakani.

Katika siku ya pili ya maandamano nchini humo, maafisa usalama walitumia gesi ya kutoa machozi na risasi za moto kuwatawanya watu jijini Kampala nchini humo.

Waandamanaji wamekuwa wakichoma magurudumu na takataka na kufunga barabara jijini Kampala. Biashara zimefungwa na askari wengi wameonekana barabarani

Akaunti ya Twitter ya Bobi Wine imeonesha watu wasio na sare wakipitapita mjini, wakifyatu risasi hewani.

One comment

Comments are closed.