Viongozi wa Umoja wa Ulaya jioni hii wanatarajiwa kuziwekea shinikizo Hungary na Poland, baada ya nchi hizo kutumia kura ya turufu kupinga maamuzi muhimu kuhusiana na bajeti ya muda mrefu ya umoja huo na mpango wa kuufufua uchumi kutokana na janga la virusi vya corona.
Viongozi wa nchi 27 wa nchi na serikali wanafanya mkutano kwa njia ya video. Viongozi hao watazishawishi Hungary na Poland kuwachana na upinzani wake kwa mfumo mpya wa utaratibu wa sheria ambao nchi hizo mbili zinauona kama unawezesha uingiliaji mkubwa wa masuala ya ndani ya nchi.
Mapema leo, mkuu wa Benki Kuu ya Ulaya Christine Lagarde ametoa wito wa kuidhinishwa bila kuchelewa mfuko wa Umoja wa Ulaya wa fedha za kuuokoa uchumi ulioharibiwa na janga la virusi vya Corona.
Mpango huo wa kifedha wa euro trilioni 1.8 utajadiliwa leo, lakini maafisa hawatarajii kupatikana suluhisho wiki hii.