Je rais Trump anapata faida gani kwa kukataa kushindwa na Joe Biden?

Rais wa Marekani , Donald Trump, amekuwa akifanya kitu kimoja tu kwa muda wa wiki mbili tangu uchaguzi ufanyike : kutoa madai bila kuwa na ushahidi kwamba aliibiwa kura zake za urais.

Licha ya ukweli kwamba mgombea hasimu wake wa chama cha Democratic, Joe Biden, alipata kura za kutosha za wapiga kura tangu Jumamosi za kuchukua kiti chake, Trump amekataa kata kata kufuata utaratibu uliozoeeleka wa kukubali ushindi huo mbele ya umma.

Licha ya kuonekana mara chake mbele ya umma na kwenda kucheza gofu katika klabu yake ya kibinafsi ya Virginia rais huyo amekuwa katika White House tangu usiku wa uchaguzi, na bila shaka akikabiliwa na wakati mgumu .

Lakini Trump ameandika na kutuma ujumbe zaidi ya 400 wa twitter na kuushirikisha umma , na ‘retweet’ za watu wengine, nyingi zikiwa ni za kupinga matokeo ya uchaguzi. Ingawa kuna wakati alikaribia kukubali ushindi wa Biden siku ya Jumapili alipoandika : “Alishinda kwasababu …”

Kama ilivyotarajiwa bila shaka, aliongeza maeneo yake kwamba ” kulikuwa na wizi wa kura katika uchaguzi ” na, muda mfupi baadaye, alifafanua kauli hiyo katika tweet nyingine kuwa: Sitoi uhakika wowote! Tuna njia ndefu bado .”

Wataalamu wengi wanasema kwamba Trump anaweza kurudisha nyuma matokeo ya uchaguzi ingawa timu yake ya wanasheria wanadai hadi sasa kwamba hakuna ushahidi wowote wa wizi wa kura, hususan baada ya wataalamu na maafisa wa uchaguzi kutoa kauli ya pamoja kwamba uchaguzi huo “ulikuwa salama kuliko uchaguzi mwingine wowote ule katika historia ya Marekani “.

Hatahivyo baadhi yao wanaonya kuwa huenda rais wa sasa wa Marekani analenga malengo mengine madogo.

”Ninadhani kuna sababu kadhaa zinazomfanya Trump akatae kukubali kushindwa na kutoa tuhuma za uongo za wizi wa kura miongoni mwake ni kwamba kuna motiosha ya kifedha ” anasema Brendan Fischer, mkurugenzi wa mageuzi ya taifa katika kituo cha kisheria cha kampeni cha Marekani, ambacho ni kikundi kinachopigia debe uwazi katika uchaguzi.

1. Faida ya pesa

Tangu ulipofanyika uchaguzi, kampeni ya Trump imekuwa ikituma makumi ya ujumbe wa barua pepe na simu ya mkononi kwa wafuasi wake wakiomba pesa kwa ajili ya “mfuko wa kulinda kura.”

Lakini Fischer anasema pesa hizo kwa kiasi kikubwa haziwezi kutumika kupambana na “ufisadi,” kulipia hesabu ya upya ya kura au mapambano ya kisheria kwani timu za kampeni za Trump na kamati ya Republican wana fedha tofauti kwa ajili ya shughuli hiyo.

Partidarios de Trump
Maelezo ya picha,Timu ya kampeni ya Trump imekuwa ikichangisha fedha kutoka kwa wafuasi wake baada ya uchaguzi

Timu ya kampeni ya Trump imetangaza kubuniwa kwa tume ya kuchukua hatua za masuala ya uchaguzi kama kitendo cha kawaida na kilichopangwa awali.

“Rais alikuwa anapanga kufanya hili, ashinde au ashindwe ,ili kuwasaidia wagombea na masuala ambayo yanamuhusu, kama vile kupambana ufisadi katika uchaguzi,” alisema msemaji wa mkurugenzi wa kampeni ya Trump Tim Murtaugh.

Kwa upande mwingine, kila mgombea ambaye Trump anataka aendelee kuwa katika siasa baada ya kuondoka, White House.

Joe Biden
Maelezo ya picha,Biden tayari anaandaa serikali yake, licha ya Trump kukataa kukubali ushindi wake

2. Mamlaka

Na ingawa Biden alipata takriban kura milioni sita kumliko, kura milioni 73 alizozipata rais zinaashiria kuwa ataendelea kuwa na ushawishi ndani ya chama cha Republican.

Baadhi ya wataalamu wanaamini kuwa kukataa kwa Trump kuukubali ushindi wa Biden pia ni nia ya kutaka kuendelea kuwahamasisha wapiga kura wake, labda kwa ajali ya wazo lake kutaka kugombea tena urais mwaka mwaka 2024.

Miles de partidarios de Trump marcharon por las calles de Washington D.C. este sábado.
Maelezo ya picha,Maelfu ya wafuasi wa Trump waliandamana katika mitaa ya mji DC Jumamosi

Licha ya kukosa ushahidi wa wizi wa kura nusu au (52%) ya Warepublican wanaamini kuwa Trump “alishinda kihalali” uchaguzi, kwa mujibu matokeo ya kura ya maoni iliyoendeshwa na Reuters / Ipsos .

Maafisa wa kikosi cha mkakati cha rais walipinga madai ya ufisadi bila ushahidi na kusema kuwa yatachunguzwa sana katika hesabu ya marudio tarehe 5 mwezi Januari katika Georgia wa viti vya urais na seneti.

Kama Wademokrati watachukua viti kutoka kwa Warepublican, Wademocrat pia watakuwa na wingi wa viti katika bunge la congresi, zadi ya bunge la wawakilishi ambo tayari wamepata udhibiti.

Trump jugando al goflf.
Maelezo ya picha,Gofu ni moja ya sababu chache zinazomfanya trump aondoke White House tangu ufanyike uchaguzi

Ni jambo gumu kujua ni lini Trump atakubali wazi ushindi wa Biden

Je atafanya hivyo hivyo baada ya majimbo kuidhinisha matokeo ya uchaguzi wao katika kipindi cha wiki kadhaa zijazo?

Labda wakati wajumbe watakapochagua rasmi rais ajaye Disemba 14? Au ataepuka kabisa kukubali kushindwa na Biden daima?.

Hakuna anayefahamu hilo isipokuwa yeye.

Ukweli ni kwamba Biden alianza kuongeza shinikizo dhidi ya Trump,kwa mfano alionya kwamba kukataa kusaidia mpango wa makabidhiano ya mamlaka kwa Trump kunaweza kuathiri vibaya mapambano dhidi ya virusi vya corona ambavyo tayari vinakadiriwa kuwauwa zaidi ya watu 250,000 nchini Marekani.

“Watu zaidi wanaweza kufa kama hatushirikiani ,”alisema rais huyo mteule Jumatatu.

Kadri muda mrefu unavyopita, ndivyo Trump anavyoupima pia ufuasi wa wakuu wa Republican ambao wameepuka kumpinga wazi. Na pia anawapima wapiga kura wa chama hizo.

Kwa yote haya anayoyafanya Trump baada ya matokeo ya uchaguzi, mchezo wa kamali anaoucheza Trump unaonekana kuwa na uwezekano wa kusababisha hatari kadhaa zadi ya faida anazoweza kuzipata.